Mashambulizi yawaua watu 3 Iraq

Watu watatu wameuawa katika mji wa Zubaidiya nchini Iraq kufuatia mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa katika gari.

Vifo hivyo vimekuja siku moja baada ya watu arobaini kuuawa katika milipuko ya mabomu nchini humo.

Mashambulio hayo yamefanyika kabla ya kuanza kwa sherehe za kidini za madhehebu ya Shia nchini Iraq.