Jeshi la Uingereza labana matumizi

Jeshi la Uingereza leo linatarajia kusikiliza litapoteza vikosi vingapi katika mpango wa taifa hilo wa kubana matumizi utakaolifanya jeshi hilo kupunguza askari wake kwa asilimia ishirini.

Takriban askari elfu themanini na mbili watapunguzwa katika jeshi hilo , kiwango hicho kikiwa ni sawa na nusu ya wale waliokuwepo wakati wa vita baridi .

Waziri wa ulinzi wa Uingreza , Philip Hammond, atalieleza bunge ni idara zipi za jeshi zitaondolewa , ikiwa ni pamoja na baadhi ya idara za kihistoria za mapigano ya Waterloo, miaka karibu mia mbili iliyopita.

Inadhaniwa kuwa batalioni tano mpya zaidi zitafutwa.