Raia wa Thailand wastakiwa Burma

Polisi  wa Burma Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wa Burma

Shirika la habari nchini Burma limesema raia kadhaa wa Thailand watafikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kuvuka mpaka na kufanya kazi katika mashamba makubwa nchini humo.

Raia sitini na moja wa Thailand, wengi wao wakiwa wanaume walikamatwa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa gazeti la New Light mjini Myanmar, raia hao walikuwa wakulima wa mashamba makubwa na kuwa walimiliki silaha kinyume cha sheria.

Lakini serikali ya Thailand imesema wakulima hao waliamini kuwa walikuwa na kibali cha kuendeleza shughuli za kilimo katika eneo hilo.