Saudia kupeleka wanawake Olimpiki

Image caption Afisa wa Olimpiki Saudia

Kwa mara ya kwanza katika historia, Saudi Arabia itaakilishwa na wanariadha wa kike katika michezo ya olimpiki itakayoandaliwa mjini London.

Ripoti zinasema wanariadha hao watashiriki katika mashindano ya Judo na riadha.

Bi Wojdan Ali Seraj atashiriki katika judo na Sarah Attar atashiriki katika mbio za mita 800 kwa akina dada.

Nchi za Qatari na Brueni ambazo miaka yote zimekuwa hazitumi wanariadha wa kike kushiriki mashindano ya kimataifa nazo zimetangaza kuwa zitawashirikisha wanawake katika timu zao.