Ajali ya gari moshi lauwa Afrika Kusini

Image caption Gari moshi lafanya ajali Afria Kusini

Maafisa nchini afrika kusini wanasema takriban watu 19 wameuwawa baada ya gari moshi kugonga lori lililokuwa limebeba wafanyikazi kwenye kivukio cha reli.

Ajali hiyo imetukia katika mkoa wa mashariki wa Mpumalanga.

Habari kamili kuhusu ajali hiyo bado hazijulikani kikamilifu.

Ingawa kuna taarifa nyengine ambazo zinasema kuwa watu wapatao 24 huenda wameuwawa.