Waasi wa Syria wakaribia Damascus

Makundi ya wapigajani nchini Syria yanasemekana kukaribia mji mkuu Damascus.

Kwa mara ya kwanza, majeshi ya serikali pamoja na magari ya kivita yanashika doria katika mji wa katikati mwa Syria wa Midan, kulinda mji mkuu dhidi ya mashambulizi.

Katika siku mbili zilizopita, vikosi vya serikali vimekabiliana na wapiganaji wanaopinga serikali, katika eneo la kusini mwa mji.

Wanaharakati wanasema kuwa barabara inayoelekea katika uwa nja wa ndege ilifungwa kwa muda mfupi leo.