Uchumi wa Dunia mashakani

Shirika la fedha duniani, IMF, limesema kuwa kuna mdororo wa uchumi wa dunia kuliko ilivyokua hapo awali licha ya juhudi za kuuchepua kushika kasi.

Katika ripoti yake ya hivi karibuni, shirika hilo linasema linashuhudia ukuaji wa uchumi ingawa bado kuna changamoto ambazo zinatishia ukuwaji huo hususan barani Ulaya na Marekani.