Maghala ya silaha ni tisho la usalama

Ripoti moja ya Umoja wa mataifa iliyofichuliwa kuhusu Somalia , imeelezea hofu ya maghala ya silaha yanayoelea kwenye ufuo wa pwani ya Afrika. Rip[oti hiyo inasema kuwa maghala hayo huenda yakawa tisho kwa usalama barani humo.

Maghala hayo yanamilikiwa na makampuni ya kibinafasi ya usalama.

Kwa usaidizi wa stima ya kuvuta meli kubwa, Maghala hayo hutumiwa kusambazia na kuhifadhi silaha na zana nzito za kivita kutoka maeneo ya baharini.

Silaha hizo zinasemekana hupelekwa katika nchi zozote kunakohitajika silaha.

Ingawa makampuni binafsi ya usalama, yamesaidia kupunguza visa vya uharamia katika eneo hilo, ripoti hiyo ya umoja wa mataifa, inasema kuwa ikiwa maghala hayo hayatadhibitiwa vyema basi huenda yakatishia usalama wa kikanda badala ya kuwa suluhisho kama ilivyokuwa nia yake.