Mshukiwa wa Nazi akamatwa Budapest

Waendesha mashtaka nchini Hungary wanasema mtu mwanaume mwenye umri wa miaka tisini na saba aliyeshukiwa kuhusika katika mpango wa kuwafukuza wayahudi kuondoka nchini humo mwaka 1944, amekamatwa nchini Budapest.

Wamesema mtu huyo Laszlo Csatary, ameshitakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Laszlo Csatary anashutumiwa kwa kusaidia mauaji ya karibu wayahudi elfu sitini katika sehemu ambayo kwa sasa inajulikana kama jiji la Kosice nchini Slovakia.

Siku ya Jumatatu kituo cha taasisi ya Simon Wiesenthal, kinachojaribu kuwaleta katika haki wahalifu wa vita vya ubaguzi wa rangi vya Nazi, kimetaka nchi ya Hungary kuwasalimisha washutumiwa wake wanaosakwa baada ya gazeti moja la Uingereza kuripoti kuwa lilimuona mshukiwa huyo huko Budapest.