Ujerumani kuongeza fedha kwa wakimbizi

Mahakama ya katiba nchini Ujerumani imetoa hukumu kuwa kiwango cha fedha za mafao zinazotolewa na serikali kwa wakimbizi ni kidogo sana na imeamuru kiongozwe kwa asilimia hamsini.

Mahakama hiyo imesema kuwa kiwango cha sasa cha dola kumi tu kwa siku hakiwezi kukidhi kile kinachokusudia kuwa msaada kwa mahitaji muhimu ya kibinaadam.

Hukumu hiyo imeitaka serikali kutunga sheria ya kuongeza kiwango hicho hadi kufikia euro mia tatu na thelathini na sita kwa mwezi, kutoka kiwango cha sasa cha euro mia mbili na ishirini na nne.

Shirika la haki za binaadam la Amnesty International limeunga mkono hukumu hiyo.