Urusi yajibu nchi zinazoikosoa kwa Syria

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa urusi amesema kuwa, ni jambo lisilokubalika kabisa kwa hatua ya mataifa ya magharibi kukosoa uamuzi wa Urusi kupiga kura ya turufu dhidi azimio la Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Alexander Lukashevich amesema badala ya kukosoa nchi yake, mataifa ya magharibi yanastahili kuwashawishi wapinzani nchini Syria kukomesha mapigano na kuanzisha mazungumzo na Damascus.