Mabomu yanyeshea Iraq

Haki miliki ya picha s
Image caption Mabubu yanyeshea Iraq

Msururu wa mashambulio katika sehemu mbalimbali nchini Iraq, uliolenga pakubwa vikosi vya kijeshi, umepelekea vifo vya takribani watu themanini na tisa kuuawa.

katika wingu hilo la mashambulizi wengine mia mbili kujeruhiwa.

Hii ni siku mbaya zaidi za ghasia nchini humo tangu vikosi vya wanajeshi wa Marekani kuondoka.

wakati wa mashambulizi hayo, polisi wa barabarani na kambi za wanajeshi zimevamiwa kwa mabomu.

Maafisa wamekaririwa wakisema baadhi ya mashambulio hayo yamefanyika katika maeneo jirani na waumini wa Kiislam wa madhehebu ya Sunni, kilomita ishirini kaskazini mwa Bagdhad.