watoto hatarini katika vita Syria

Shirika la hisani la Uingereza, la War Child, limesema pande zote zinazohusika na mgogoro nchini Syria kwa makusudi wanawalenga watoto ambao wanakabiliwa na vitendo vya mauaji, kujeruhiwa vibaya, kutekwa na kubakwa.

Katika kile shirika hilo linachokieleza kuwa ni uchunguzi wa kina wa mgogoro kuhusu watoto, limezishutumu pande zinazopingana kwa kuwaorodhesha watoto kuwa askari wapiganaji na kuwatumia kama ngao.

War Child linaonya kuwa hakuna mtoto ambaye ni salama kwa sasa nchini Syria, ikiwa ni pamoja na watoto wanaokadiriwa kufikia milioni mbili katika mji mkuu Damascus.