Misri yapata Waziri Mkuu Mpya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mohammed Mursi ateuwa waziri mkuu

RAIS mpya wa Misri, Mohammed Mursi, amemteua waziri wa maji, Hisham Kandil, kama Waziri mkuu.

Kufuatia uteuzi huo sasa Rais Mursi amemuamuru Khandil kuunde serikali.

Hadi kufikia sasa Bwana Kandil hakuwa na sifa kubwa au umaarufu nchini Misri. Na pia hatoki katika vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo Rais Mursi ni mwanachama wake.

Rais Mursi alikuwa ameahidi serikali