Waasi wa Ethiopia waitisha kongamano

Makundi ya waasi nchini Ethiopia yameitisha kongamano la wazalendo wote yakisema ni hatua ya kuleta mageuzi ya kidemokrasia.

Taarifa hii imetolewa na makundi ya Oromo, Somali na Sidama wakati afya ya kiongozi wa nchi Meles Zenawi ikiripotiwa kuendelea kuzorota.

Makundi hayo ya waasi yameendeleza harakati zao dhidi ya serikali ya sasa tangu kutwaa madaraka mwaka 1991. Yamesema nia yao ni kutatua matatizo ya nchi hio ambayo yamekuwepo kwa miongo miwili.

Waasi hao wamekua wakiwalenga wanajeshi wa serikali katika maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi.