Mauzo ya Japan yaanguka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mauzo na biashra nchini Japan

Japan imerekodi kiwango kikubwa kabisa cha nakisi ya biashara kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi sita ya mwaka huu.

upungufu huo unakisiwa kukaribia dola bilioni arobaini.

Sababu kubwa ilikuwa ni kuagiza mafuta na gesi asilia kwa ajili ya uzalishaji wa umeme baada ya kuzimwa kwa mitambo ya nyuklia.

Ni mitambo miwili tu kati ya sitini na mbili ambayo imewashwa tena baada ya kuzimwa ili kukagua hali ya usalama katika mitambo hiyo kutokana na ajali ya nyuklia katika mitambo ya Fukushima iliyotokea mwezi Machi mwaka jana.

Kuyumba kwa uchumi katika mataifa ya Ulaya na kusuasua kwa uchumi wa Uchina na kuimarika kwa sarafu ya Yen ni miongoni mwa sababu zilizosababisha kushuka kwa biashara ya Japan.