wakuu 12 kushitakiwa Nigeria kwa ufisadi

Waendesha mashitaka nchini Nigeria ambao wanachunguza ufisadi katika sekta ya mafuta, wanasema watawashitaki watu 12 katika sakata hiyo.

wakuu hao pia wamesema watizishitaki kampuni saba kwa wizi wa dola milioni 70 kupitia ukiukwaji wa mpango wa ruzuku ya mafuta.

Waendesha mashitaka hao dhidi ya ufisadi wametangaza kufungua mashitaka hayo kufuatia uchunguzi wa bunge ambao ulibainisha kuwa Nigeria imepoteza karibu dola bilioni saba kutokana na mapato ya mafuta tangu mwaka 2009 kutokana na vitendo vya rushwa katika sekta hiyo.