China yasema 77 walifariki mafurikoni

Image caption mafuriko nchini china

Baada ya shinikizo za siku tano hatimae, serikali ya China imesema idadi ya watu waliofariki kutoka na mvua kubwa na mafuriko ni watu 77.

Mwishoni mwa wiki mvua kubwa ilishuhudiwa mjini Beijing ambapo wakuu wa serikali walidai ilisababisha vifo vya watu 37.

Lakini baada ya shutma kutoka kwa raia wa china, hatimae Serikali leo kupitia idhaa ya serikali imetangaza kuwa idadi waliokuwa ni 77 na wala sio 37.