Korea Kaskazini wagomea Olimpiki

Haki miliki ya picha AP
Image caption Korea Kusini wagomea mechi ya Olimpiki

Timu ya kandanda ya wanawake kutoka Korea kaskazini waliondoka uwanjani kabal ya mechi ya ufunguzi ya mashindano ya Olimpiki mjini London baada ya ya bendera ya Korea kusini kupeperushwa kimakosa kando ya majina ya wachezaji katika runinga ya uwanjani.

Mechi hio dhidi ya Colombia katika mji wa Glasgow ilicheleweshwa kwa zaidi ya saa moja.

Mechio hio iliendelea baada ya waandaji wa michezo hio ya Olympiki kuomba msamaha, na Korea Kaskazini wakashinda kwa mabao mawili kwa nunge.

Kumwkuwa na uhasama kati ya Korea kusini na Kaskazini tangu kusitishwa vita dhidi ya nchi hizo mbili manmo mwaka wa 1953.