Thamani ya hisa za Facebook yashuka

Thamani ya hisa za tovuti mashuhuri ya kijamii - Facebook zimeshuka kwa kiwango cha asilia mia nane, kufuatia kuchapishwa kwa mara ya kwanza, matokeo ya utenda-kazi wake tangu kampuni hio iamue kuwa kampuni ya umma mnamo mwezi Mei.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya biashara amesema kuwa wawekezaji wana wasiwasi kuwa kampuni hio bado haijabuni njia muafaka ya kufaidi kutokana na mashabiki wanaoendelea kuongezeka katika tovuti yake kupitia kwa simu.

Mwanzilishi wa tovuti hio ya Facebook, Mark Zuckerberg, aliwaambia wawekezaji kuwa matangazo ya kibiashara yanafaa kumpa mtumiaji wa tovuti hio .