Romney ahudhuria ofunguzi wa olimpiki

Baada ya Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Mitt Romney, kusema kuwa ana wasiwasi juu ya utayari wa Uingereza kuandaa michezo ya Olimpiki sasa anajitahidi kupooza moto aliouwasha.

Hii ni baada ya waziri Mkuu wa Uingereza kumjibu kwa kusema kuwa amshindano hayo yanaweza kuandaliwa mahali popote na Uingereza iko tayari.

Sasa Romney yuko uingereza akijiandaa kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo

Lakini baada ya kumtembelea waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, Bw Romney alisema kuwa ana matumanini makubwa michezo hio itafanikiwa.