M23 wasakamwa zaidi na Umoja wa Mataifa

Umoja wa mataifa umesema kuwa vikosi vyake katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vimesaidia katika kuwafurusha waasi wa kundi la M23 kutoka kwa miji miwili - ilio mashariki mwa nchi hio.

Helikopta za kivita zilitumika katika operesheni hio inayo viunga mkono vikosi vya wanajeshi wa kitaifa katika miji ya Rugari na Rumangabo, kaskazini mwa mji wa Goma.

Waasi wa kundi la M23 wamekuwa wakiusogelea mji wa Goma katika mashariki mwa Congo.

Umoja wa mataifa umeituhumu serikali ya Rwanda kwa kuwafadhili waasi hao, lakini Rais wa Rwanda Paul Kagame amepuuza madai hayo. Zaidi ya watu laki mbili unusu wamefurushwa makwao na