Mwanamke Vietnam ajichoma moto

Mwanamke mmoja wa Ki-Vietnam anaripotiwa kufa kwa majeraha ya moto baada ya kujichoma mwenyewe mbele ya ofisi ya serikali ya mtaa.

Ndugu mmoja wa familia amesema alikuwa anapinga kitendo cha binti yake kuzuiliwa kwa tuhuma za kupinga propaganda za nchi.

Amesema alikufa akiwa anapelekwa hospitali mjini Ho Chi Minh.

Binti wa mwanamke huyo Ta Phong Tan, alikuwa polisi na mwana blogu ambaye alizuiliwa mwaka jana baada ya kuonyesha vitendo vya kikatili na unyanyasaji vinavyofanywa na polisi.