Mamia ya mamilioni India wakosa umeme

Mamia ya mamilioni ya watu wameachwa bila umeme kaskazini na mashariki mwa India baada ya kutokea hitilafu kubwa ya mitambo yake.

Zaidi nusu ya nchi ilikumbwa na kukatoka kwa umeme baada ya maeneo matatu ya gridi ya Taifa kushindwa kufanya kazi moja ikiingia sikuya pili.

Treni kwa mamia nchini humo zimesitisha safari zake na hosptali zinaendeshwa kwa majenereta.

Waziri wa nishati ameshutumu serikali kwa kuchukua umeme mwingi kutoka kwenye grid ya Taifa.

Kukatika kwa umeme kaskazini mashariki na kaskazini mashariki kuna maanisha kuwa karibu watu milioni mia sita wameathiriwa na hali hiyo katika majimbo 20 ya India.