Maelfu wanaswa kwenye mapigano Aleppo

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa maelfu ya watu bado wamenaswa mjini Aleppo mji wa kibiashara nchini Syria huku mapigano makali yakiendela kwa siku ya nne.

Wanaharakati wanasema mji huo unaanza kupungukiwa na mahitaji muhimu ya chakula na gesi ya kupikia

Mapigano mapya yamekuwa yakiendelea na mashambulizi ya helkopta yameripotiwa lakini waasi wanasema wanaendelea kushikilia wilaya Salah al-Din.

Umoja wa Mataifa unasema watu 200,000 wamekimbia mapigano mjini humo.

Lakini Melissa Fleming, msemaji wa UNHCR anasema wengi zaidi wanashindwa kuondoka kwa sababu kufanya safari au wanahisi itakuwa hatari sana.