Wachezaji waliodanganya wafutwa Olimpiki

Shirikisho la mchezo wa vinyoya duniani limewafuta kwenye michezo ya olimpiki inayoelendele mjini London.

Wachezaji wanane wa mchezo wa vinyoya walituhumiwa kupoteza mchezo kwa makusudi ili waweze kuingia katika hatua ya robo fainali kwa upande wa wanawake.

Wachezaji hao wanne kutoka Korea ya Kusini, wawili wa china na wawili wa Indonesia walizomewa na mashabiki waliokuwepo uwanjani walipokuwa wakicheza kwa kupanga matokeo.

Mwenyekiti wa kamati ya kuratibu mashindano ya Olympiki Lord Coe amesema kitendo walichokifanya kinadidimiza na ni habari mbaya kwa michezo.

Tayari China ilishatangaza kufanya uchunguzi kwa wachezaji huku Shrika la habari la taifa la China imewalaumu wachezaji hao na walipaswa kucheza kama ilivyopaswa kuliko kuangalia zaidi kupata medali ya dhahabu.