Kampuni ya Nyuklia Japan yapata hasara

Mtambo wa nyuklia wa Fukushima nchini Japan umepoteza dola bilioni tatu nukta saba katika robo ya mwisho ya mwaka wa fedha.

Kampuni inayoendesha mtambo huo inakabiliwa na ongezeko la gharama za uharibifu uliotokea mwaka jana.

Shirika la Umeme la Tokyo TEPCO, linakabiliwa na ankara kubwa ya kurekebisha na kulipa fidia madai ya watu waliokosa makazi baada ya ajali ya Fukushima iliyosababishwa na tsunami mwezi Machi.

Kampuni hiyo pia inakiwa kutoa fedha za mafuta mbadala ili kukidhi mahitaji ya nishati baada ya kufunga mitambo yake iliyobaki.

TEPCO inapata dola bilioni 13 kila wiki na ilikiri mapema makadirio ya kurejea katika hali ya kawaida ilikuwa ni ndoto.