Kesi ya wanamuziki yavurugika Urusi

Kesi ya wanamuziki watatu wa Urusi wa kundi la Pussy Riot lililodaiwa kumkashifu rais wa nchi hiyo Vladimir Putin imevurugiga baada ya mmoja wa wanamuziki hao kuugua.

Mwanasheria wa wanamuziki hao alisema Maria Alyokhina amepatwa na tatizo la kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu huku akisema hiyo inatokana kutokula vizuri.

Wandamanaji wamekuwa wakiwashutumu wanamuziki hao kwamba waliimba mambo ya kipuuzi katika madhabahu ya kanisa.

Kesi hiyo imesababisha ukosoaji mkubwa kutoka kwenye makundi haki za binadamu.

Itaendelea tena.

Mwandishi wa BBC mjini Moscow anasema wanawake wamesafiri hadi kwa saa nne kuja mahakamani ikimaanisha kuwa walikuwa na muda mdogo wa kulala.