Usain Bolt kupokea medali yake leo

Mwanariadha mashahuru wa Jamaica, Usain Bolt anatarajiwa kupokea medali yake ya dhahabu hii leo baada ya kushinda fainali ya mbio hizo mnamo Jumapili

Sherehe ya kukabidhiwa medali hiyo kwa Bolt zinafanyika wakati mmoja na maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru wa Jamaica.

Akiwa na mwanaridaha mwenzake ambaye alishinda fedha katika mbio hizo, Yohan Blake, ushindi wa Bilt ulithibitisha kuwa yeye ndiye mwanaridha mwenye kasi kubwa kushinda wote duniani.

Tayari sherehe zimeanza kufanyika nyumbani Jamaica kama ishara ya furaha ya ushindi wa Bolt.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria sherehe za maadhimisho ya uhuru wa Jamaica.