Roboti ya NASA yatua kwenye Mars

Shirika la Marekani la Utafiti wa Anga za Juu, NASA, linasherehekea kutua salama kwa chombo chake cha utafiti cha roboti katika sayari ya Mars, kufuatia safari iliyodumu kwa miezi tisa.

Wafanyakazi katika kituo cha NASA huko California walishangilia na kukumbatiana, baada ya chombo hicho kutua katika sayari ya Mars.

Chombo hicho chenye uzito wa tani moja kilishushwa taratibu na mwavuli na roketi ili kuhakikisha kinatua salama.

Dakika chache baada ya kutua kikaanza kutuma picha za sayari ya Mars.

Lengo la kupelekwa chombo hicho ni kutafiti taarifa iwapo sayari hiyo inawezesha viumbe kuishi.