Majeshi ya Syria yashambulia Allepo

Majeshi ya serikali ya Syria yameimarisha makabiliano katika mji wa Aleppo kwa mashambulio makali dhidi ya ngome kuu za waasi.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema kuwa kasi ya mashambulizi yanayofanywa na majeshi ya serikali kutumia vifaru na ndege za kivita imeongezeka sana.

Wanaharakati wa upinzani wametoa picha za video kuonyesha majeshi hayo yalivyochoma majengo na mali za watu ambayo wamesema pia mashambulio mengi yalifanywa kwa ndege za kivita.

Shirika la habari la Syria nalo limeripoti kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio la bomu katika ofisi zake mjini Damascus.