Kambi ya NATO yashambuliwa Afghanistan

Maafisa nchini Afghanistan wanasema mshambuliaji wa kujitolea mhanga ameshambulia kituo cha majeshi ya NATO na kujeruhi raia kumi na mmoja wa Afghanistan na wanajeshi wawiwili wa kigeni.

Mshambuliaji huyo alitumia Lori iliyokuwa imebeba vilipuzi kulenga kituo hicho ambacho kilo katika jimbo la Logar .

Watu walioshuhudia wanasema walisikia mlipuko mkubwa kwa umbali wa kilomita kadhaa.

Katika shambulizi lengine lililotokea hapo awali viungani mwa mji wa Kabul, polisi walisema kuwa watu tisa waliuawa.

Watu hao walikuwa wansafiria kwenye basi ambako gari hilo lilipogonga bomu hilo na kisha kulipuka.