Mtoto afariki akipungwa mapepo Malaysia

Polisi nchini Malaysia, wanasema kuwa mtoto mwenye umri wa miaka mitatu alifariki nyumbani kwao wakati familia yake ikimfanyia tambiko la kumpunga mapepo ambalo halikufanikiwa kama walivyotarajia.

Kwa mujibu wa polisi katika jimbo la Penang , kaskazini mwa nchi, waliitwa kwenye nyumba hiyo baada ya mmoja wa jamaa za mtoto huyo kushikwa na na wasiwasi .

Katika nyumba hiyo polisi walipata watu wazima wanane ikiwemo mamake mtoto huyo, mfanyakazi wa nyumbani mwenye uraia wa Indonesia wote wakiwa wamejifungia ndani ya chumba wakiwa wamemlalia mtoto yule na kujifunika mablanketi.

Watu hao, walikuwa wamejifunika kwa blanketi wakiwa wanaimba nyimbo kwa kurudiarudia. Kulingana na polisi, kitendo hicho inaarifiwa kilikuwa kimedumu kwa muda mrefu.