Rais wa Korea Kusini na ziara ya utata

Rais wa Korea Kusini Lee Myung-bak ametembelea visiwa ambavyo Japan pia inadai kuwa ni eneo lake, hatua ambayo huenda ikaleta mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Lee Myung-bak ametembelea visiwa hivyo vinavyojulikana kama Dokdo Korea Kusini na pia kujulikana kama Takeshima nchini Japan.

Shirika la habari la Kyodo limesema Japan imemrudisha nyumbani balozi wake aliyekuwa Korea Kusini.

Korea Kusini na Japan kwa pamoja wanasema wamekuwa na madai ya kihistoria juu ya visiwa hivyo na suala hilo limekuwa ni la muda mrefu likiathiri uhusiano wa nchi hizo mbili.

Visiwa hivyo kati ya nchi hizo mbili ni vidogo lakini vikiwa katika sehemu ambayo ni muhimu kwa uvuvi na huenda vikawa rasilimali kubwa ya gesi.