Rais wa Misri aomba kuungwa mkono

Rais wa Misri Mohammed Mursi, ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kumuunga mkono, kufuatia hatua yake ya kumfuta kazi kamanda wa jeshi la taifa hilo aliye na ushawishi mkubwa.

Wafuasi wa Rais huyo, wa mrengo wa kiislamu, wameshangilia hatua hiyo ya kumfuta kazi Field Marshal Mohamed Hussein Tantawi, na wengi wanasema hatua hio inaashiria kuwa mchakato wa mageuzi umefikia upeo wa juu.

Rais Mursi pia amefutilia mbali mabadiliko ya katiba yaliotekelezwa na jeshi yaliyopunguza mamlaka yake ya urais. Morsi alisema kuwa hakuwa na nia ya kuwalenga watu binafsi au ku-aibisha taasisi yoyote ile kufuatia uamuzi wake.