Uchumi wa ulaya wazidi kuzorota

Imebadilishwa: 14 Agosti, 2012 - Saa 19:43 GMT

Uchumi wa nchi za ulaya unaonyesha kuendelea kushuka licha za jitahada za kuimarisha uchumi huo.

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa, kwa ujumla ukuaji uchumi katika nchi kumi na saba zinazotumia sarafu ya Euro umeshuka kwa asilimia sifuri nukta mbili katika miezi mitatu iliyopita.

Mwandishi wa BBC katika masula ya Ulaya, anasema viongozi wa nchi za Ulaya wanaonekana kushindwa kudhibiti kuzorota kwa uchumi wa nchi hizo huku wasiwasi zaidi ukiongezeka juu ya mzigo wa madeni.

Kukosekana kwa ukuaji katika uchumi kutafanya kuwa vigumu kwa nchi za ulaya ambazo tayari uchumi wake uko matatani.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.