Mahakama yaidhinisha uamuzi wa serikali

Imebadilishwa: 15 Agosti, 2012 - Saa 15:18 GMT
Pakiti ya Sigara

Pakiti ya Sigara

Shirika Afya Ulimwenguni, WHO, limeafiki uamuzi uliotolewa na mahakama kuu nchini Australia, wa kufutilia mbali rufaa iliyowasilishwa na kampuni kubwa za kutengeneza bidhaa za tumbako, na wakati huo huo kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kufuata mfano huo wa Australia kuhusu uuzaji wa bidhaa za tumbako.

Kampuni kubwa za kutengeneza bidhaa za tumbako nchini Australia zilikwenda mahakamani, kupinga sheria iliyowashurutisha kuuza sigara na bidhaa zingine za tumbako katika pakiti zizizokuwa na maandishi.

Lakini jaribio la washika dau wa secta hiyo la kuhujumu kutekelezwa kwa sheria hiyo sasa imetumbukia nyongo.

Kufikia Desemba mwaka huu, Australia, itakuwa nchi ya kwanza kuuza sigara kwenye pakiti ya kijani isiyokuwa na maandishi yoyote ya kibiashara.

Kufuatia uamuzi huo secta ya afya ya umma imeingia katika awamu mpya ya kudhibiti matumizi ya bidhaa za tumbako.

Mfumo huo wa kuuza sigara kwenye pakiti zizizokuwa na maandishi ni bora zaidi kuzuia ushindani mkali ulioibuka miongoni mwa kampuni za kutengeza sigara, hatua iliyosababisha uvutaji wa sigara kuongezeka maradufu.

Sheria hiyo pia inaambatana na azimio la shirika la WHO kuhusu matumizi ya tumbako.

Rufaa hiyo iliyowasilisha na kampuni kubwa za tumbaku imeonekana kama pigo kubwa kwa secta hiyo.

Inakisiwa kuwa nusu ya watu wanaotumia bidhaa za tumbako, hatimaye huenda wakaaga dunia kutokana na matatizo yanayosababisha na utumizi wa sigara, hii ikiwa ni sawa na vifo vya watu milioni sita kila mwaka.

Shirika la WHO limeonya kuwenda endapo serikali zote hazitachukua hatua madhubuti kudhibiti matumizi ya tumbako, ifikiapo mwaka wa 2030, takriban watu milioni nane huenda wakaangamia kila mwaka.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.