Marekani yakana Israil kushambulia Iran

Imebadilishwa: 15 Agosti, 2012 - Saa 05:35 GMT

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Leon Panetta, amesema kuwa Israil haina mpango wo wote wa kushambulia Iran katika juhudi zake za kuikomesha kuendeleza silaha zake za kinukilia.

Alikuwa nchini Israil hivi majuzi ambapo alisema kuwa Marekani inachunguza mbinu zote, hata ikiwa ni kutumia wanajeshiijeshi kukomesha Iran.

Uvumi wa hivi sasa unadokeza kuwa huenda Israil ikaamua kushambulia Iran bila kushauriana na ye yote katika juhudi za kukomesha taifa hilo la Kiarabu kujistawisha kinukilia.

Hata hivyo Waziri wa Ulinzi wa Marekani Panetta, anasema kwamba Israil haijafikia hatua hiyo.

Bwana Panetta alisisitiza kuwa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekewa Iran vinaendelea kuvuruga uchumi wa taifa hilo la Kiarabu na kwamba kungali kuna uwezekano wa kuendelea na mashauriano ya kidiplomasia kuhusiana na utata huo.

Kuna wachanganuzi wa maswala ya kisiasa katika Mashariki ya Kati wanaoamina kuwa hatua itakayochukuliwa na Israil itategemea uchaguzi wa Urais wa Marekani unaotarajiwa zaidi ya miezi miwili ijayo na wala sio uwezekano wa kijeshi nchini Israil.

Rais Obama hataki kujikuta katika hali ya kutakikana kusuluhisha vita nchini Israil wakati huu ambapo kampeni ya uchaguzi imepamba moto nchini mwake. Kwa sasa Rais Obama angali anataka kuendelea na mpango wa kidiplomasia.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.