Mlipuko wa bomu waua nchini Urusi

Imebadilishwa: 19 Agosti, 2012 - Saa 19:52 GMT

Mlipuaji wa kujitolea muhanga amewauwa polisi saba na kuwajeruhi wengine katika eneo la Ingushetia nchini Urusi.

Tukio hilo limetokea katika mazishi ya afisa mmoja wa polisi aliyeuawa wakati wa ufyatulianaji risasi siku ya jumamosi.

maafisa wanasema polisi walikuwa wameingia katika nyumba iliyokuwa ikifanyika mazishi hayo wakati bomu hilo lilipolipuka.

Shambulio hilo limetokea siku moja baada ya watu waliokuwa wamefunika nyuso zao kuwajeruhi watu wanane katika msikiti kwenye eneo jirani la Dagestan.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.