Mauji ya kushtua Afghanistan

Imebadilishwa: 27 Agosti, 2012 - Saa 14:44 GMT

Maafisa wa utawala nchini Afghanistan wamesema kuwa wanamgambo wa Taliban wametekeleza mashambulizi makali zaidi dhidi ya raia katika mkoa wa Helmand - na kuwaua watu kumi na saba, wakiwemo wanawake waiwili, kwa kuwakata vichwa.

Miili yao ilipatikana leo asubuhi

Maafisa nchini Afghanistan wameelezea kuwa wanachunguza mauaji hayo.

Waathiriwa inasemekana walichinjwa na wengine kukatwa vichwa vyao.

Baadhi yao walionyesha dalili za kuchapwa vibaya na wengine wakiwa na alama za risasi.

Maafisa wa utawala wamekuwa wakitoa taarifa za kutofautiana kuhusiana na tukio hilo.

Afisaa mmoja alisema kuwa anaamini kuwa mauaji yalifanyika baada ya kutokea ubishi kati ya makamanda wawili wa Taliban.

Mapema leo, afisaa mmoja ambaye ni msemaji wa gavana wa jimbo
Daud Ahmadi, alisema kuwa wanamgambo wa Taliban walishambulia kundi moja la watu waliokuwa kwenye sherehe zao.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.