Mzozo Somalia kabla bunge kufunguliwa

Imebadilishwa: 27 Agosti, 2012 - Saa 14:08 GMT


Mzozo wa kisiasa umezuka nchini Somalia, siku mbili tu kabla ya kuzinduliwa kwa bunge la nchi hio.

Rais wa serikali ya Mpito anaeondoka madarakani, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, anasisitiza kuwa wabunge kumi na sita waliokataliwa na jopo la Umoja wa mataifa kwa sababu ya tuhuma za kuhusika kwao katika uhalifu wa kivita, wanafaa kuruhisiwa kuwakilisha watu wao bungeni.

Rais Sharif amesema atawasilisha swala hilo kwa mahakama ya juu, lakini Umoja wa mataifa, pamoja na baadhi ya viongozi wa ki-Somali, wamesema mahakama hio haina nafasi ya kulizungumzia swala hilo.

Wabunge waliokataliwa wana makundi ya wapiganaji na huenda wakatatiza serikali itayoundwa baada ya hapo kesho jumanne punde bunge likishakutana.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.