Helikopta yadunguliwa Syria

Imebadilishwa: 27 Agosti, 2012 - Saa 14:17 GMT

Makundi ya upinzani nchini Syria yamesema yameidungua helikopta ya kijeshi iliokuwa ikiwashambulia waasi katika mji mkuu Damascus.Kanda ya video imetolewa kwenye mtandao ikionyesha helikopta ikianguka chini, katika mtandao.

Kulingana na runinga ya serikali, helikopta moja ilianguka karibu na msikiti katika mtaa ulio viungani mwa Damascus. Lakini haikusema iwapo helikopta hio ilidenguliwa na waasi.

Mwandishi wa BBC amesema inaonekana helikopta hio ilikuwa miongoni mwa mashambulizi dhidi ya waasi ambapo waasi wanadai zaidi ya watu mia tatu wameuliwa katika siku za hivi maajuzi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.