Kimbunga Isaac chafika New Orleans

Imebadilishwa: 29 Agosti, 2012 - Saa 07:54 GMT

Maelfu ya watu wameutoroka mji wa New Orleans huku mji huo ukitarajiwa kupigwa na kimbunga Isaac.

Kimbunga hicho, kitapiga Louisiana miaka saba baada ya mji huo kupigwa na kimbunga Katrina, ingawa kimbunga hiki hakitakuwa cha kiwango cha juu.

Kimbunga Isaac tayari kimefika nchi kavu katika jimbo la Louisiana .

Taasisi ya mafuriko na tufani nchini Marekani imeonya kutokea mvua kubwa ya gharika hasa katika ufuo wa ghuba ya mexico.

Loiusiana imeanza kukumbwa na mvua kubwa na upepo mkali huku New Orleans wakisemekana kuweka vizuizi vya mafuriko katika mji wote.

Maelfu ya wakaazi wametorokea usalama na waliosalia wamejifungia majumbani.

Kampuni za mafuta na kusambaza gesi pia zimesitisha kwa muda oparesheni zao.

Kikosi maalum cha usalam kimetumwa huko pia kuzuia watu kupora maduka katika eneo la New Orleans, inayoaminiwa kuwa na takriban wakaazi laki tatu unusu.

Kimbunga hicho kilisababisha vifo vya takriban watu 24 kilipogonga Haiti pamoja na Jamuhuri ya Dominica.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.