Msomaji habari mwenye hijabu

Imebadilishwa: 3 Septemba, 2012 - Saa 08:46 GMT

Mwanamke aliyevalia mtandio amesoma habari za televisheni kwa mara ya kwanza nchini Misri,tangu kituo cha kitaifa kuanzishwa miaka ya tisini.

Fatima Nabil ambaye alikuwa amevalia suti nyeusi na mtandio ameielezea hatua hiyo kuwa mabadiliko makubwa.

Awali msomaji habari yeyote aliyejaribu kuvalia mtandio hakuruhusiwa kusoma habari.

Waziri wa habari wa Misri amesema kuwa thuluthi mbili ya wanawake huvalia mtandio nchini Misri.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.