Kesi ya kukufuru dini Pakistan

Imebadilishwa: 3 Septemba, 2012 - Saa 09:45 GMT

Kesi ambayo msichana mmoja wa kikristo alikamatwa nchini Pakistan chini ya sheria tatanishi ya kukufuru dini, imeakhirishwa huku msichana huyo akiendelea kuzuiliwa.

Taarifa zinasema kuwa mgomo wa mawakili ulitatiza kesi hiyo kuweza kuendelea hii leo.

Rimsha Masih alishtakiwa kwa madai ya kuchoma kurasa za Quran.

Lakini mhubiri mmoja wa kiisilamu , Khalid Chishti, amekamatwa kwa njama ya kujaribu kumlimbikizia msichana huyo makosa ambayo hakuyafanya.

Mashahidi katika kesi hiyo akiwemo msaidizi wa mhubiri huyo, aliambia wendesha mashtaka kuwa walimuona mhubiri huyo akiongeza kurasa za Quran kwenye mfuko aliokuwa anaubeba msichana huyo ukiwa na karatasi zilizochomwa.

Hatua ya msichana huyo kuzuiliwa imezua hisia kali kutoka kwa makundi ya kikristo pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu na vile vile kuna taarifa zenye utata kuhusu umri wake na hali yake ya kiakili.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.