Gari la ubalozi wa Marekani lashambuliwa

Imebadilishwa: 3 Septemba, 2012 - Saa 09:14 GMT

Shambulizi la bomu lililotegwa ndani ya gari ya ubalozi wa Marekani nchini Pakistan, limewaua takriban watu watatu mjini Peshawar.

Taarifa ya ubalozi wa Marekani zimesema kuwa wamarekani wawili na raia wawili wa Pakistan waliokuwa wanafanya kazi katika ubalozi huo walijeruhiwa vibaya.

Msemaji mmoja wa Marekani, alikanusha taarifa za awali zilizotolewa na maafisa wa usalama wa Pakistan kuwa ni raia wawili wa Marekani waliouawa kwenye shambulizi hilo .

Eneo ambalo shambulio hilo limetokea ni sehemu yenye ofisi za mashirika mengi ya kimataifa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.