'Cocain Queen' auawa nchini Colombia

Imebadilishwa: 4 Septemba, 2012 - Saa 09:47 GMT

Mlanguzi wa madawa ya kulevya nchini Colombia, anayejulikana kama "queen of cocaine", ameuawa katika mji wa Medellin.

Griselda Blanco, mwenye umri wa miaka 69, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akiondoka katika duka la kuuza nyama.

Blanco alikuwa mfanyabiashara wa kwanza wa mihadarati kuuza kiwango kikuba cha Cocain nchini Marekani katika miaka ya sabini na themanini.

Yeye ndiye aliyeimarisha njia za kusafirishia madawa hayo ambazo zimekuwa zikitumiwa na genge la mihadarati la Medellin baada ya yeye kufungwa jela kwa miaka 20, alipopatikana na hatia ya kuendesha biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Alijulikana kwa sifa yake ya ukatili, hasa baaada ya ripoti kuwa aliamuru mauaji ya washindani wake wa kibiashara ili aweze kudhibiti biashara hiyo.

Alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela na mahakama ya Marekani mnamo mwaka 1985, na kisha baadaye akarejeshwa nchini Colombia mnamo mwaka 2004.

Familia yake ilisema kuwa tangu arajee nyumbani baada ya kuhudumia kifungo chake, Blanco aliweza kukata uhusiano wake na makundi ya wahalifu.

Polisi mjini Medellin wanachunguza kifo chake na sababu za mauaji yake.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.