Wahamiaji haramu wafukuzwa Uhispania

Imebadilishwa: 4 Septemba, 2012 - Saa 09:09 GMT

Maafisa wa utawala nchini Uhispania wamewafukuza zaidi ya wahamiaji haramu themanini kutoka katika kisiwa kimoja ambacho hakikai watu katika ufuo wa pwani ya Morocco.

Msemaji wa polisi alisema kuwa wengi wa wahamiaji hao walikabidhiwa kwa maafisa wa utawala wa Morocco.

Uhusipania ilikubali kuwapa hifadhi angalau wahamiaji kumi.

Wahamiaji hao, waliwasili katika kisiwa hicho (Isla de Tierra) wiki jana na kupokea chakula na blanketi kutoka kwa polisi wa Uhispania.

Hata hivyo haijabainika walikotoka wahamiaji hao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.