Mkutano wa kisiasa washambuliwa Canada

Imebadilishwa: 5 Septemba, 2012 - Saa 08:54 GMT


Mtu aliyekuwa amejihami nchini Canada, ameshambulia kwa risasi mkutano wa hadhara wa watu waliokusanyika kusherehekea ushindi wa waziri mkuu mpya wa jimbo la Quebec na kumuua mtu mmoja huku mwingine mmoja akijeruhiwa vibaya.

Waziri mkuu huyo Pauline Marois wa chama kinachotaka uhuru wa jimbo hilo, Parti Quebecois, alitolewa kwenye ukumbi huo mara moja na walinzi wake.

Alikuwa ameelezea nia yake ya jimbo hilo ambalo wenyeji wake wengi ni wafaransa kutaka kujitenga wakati milio ya risasi iliposikika.

Mshukiwa wa uvamizi huo ambaye anasemekana kuwa na umri wa miaka hamsini alisikika akipiga mayowe akisema '' Wazungu wamejanjaruka'' huku akikamatwa na polisi.

Chama cha Parti Quebecois kilishinda viti vya kutosha katika uchaguzi wa majimbo ambavyo vinakiwezesha kuunda serikali ya wachache na kukiwezesha kurejea mamlakani baada ya karibu miaka kumi ya kudidimia kwa umaarufu wake.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.