Askari jeshi wakamatwa Afghanistan

Imebadilishwa: 5 Septemba, 2012 - Saa 13:38 GMT

Afghanistan inasema imewakamata na kuwafuta kazi mamia ya askari wa nchi hiyo kutoka jeshi la taifa kufuatia mashambulio yaliyotokea dhidi ya vikosi vya kimataifa yaliyofanywa na askari wa usalama wa Afghanistan .

Generali Zahir Azimi, kutoka wizara ya ulinzi ya Afghanstan , amesema kuna ushahidi kwamba baadhi ya askari wana uhusiano na makundi ya wanamgambo.

Zaidi ya askari arobaini wa kikosi cha NATO waliuawa na wenzao wa Afghanistan mwaka huu . Jumapili jeshi la Marekani lilisema limeakhirisha mafunzo kwa askari polisi zaidi ya elfu moja na uchunguzi mkali utafanyika .

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.